•     

Wanajeshi wa Tanzania wakiongozwa na Brig Gen Kwiligwa wako Nchini Rwanda

Kikosi cha wanajeshi wanaofanya kazi kwenye mpaka kati ya Tanzania na Rwanda wako nchini Rwanda kwa mkutano wa 10 unaowakutanisha maafisa wa usalama wa ngazi hiyo katika nchi zote mbili.

Wanajeshi wa Tanzania wakiongozwa na Brig Gen Kwiligwa wako nchini Rwanda

Jeshi la Rwanda limesema kuwa tangu Jumanne tarehe 07/05/2024 limepokea kikosi cha wanajeshi wa Tanzania wakiongozwa na Brig Jenerali Gabriel Elias Kwiligwa.

Huyu ndiye anayeongoza askari wa Brigedi ya 202 iliyopo kwenye mipaka ya Tanzania na Rwanda.

Wanajeshi hawa walipokelewa na Kanali Justus Majyambere, anayeongoza Kitengo cha 5 cha Jeshi la Rwanda, ambapo walikutana kwenye mpaka wa Rusumo.

Baadaye walikwenda kutembelea Soko la Kibare ambalo riko katika Kata ya Ndego Wilaya Kayonza, ambalo ni maarufu kwa Watanzania waishio Wilaya ya Karagwe.

Wanajeshi hawa watafanya mikutano na Wanyarwanda,  katika Wilaya ya Nyagatare, kisha kutembelea maeneo tofauti kwenye mipaka ya nchi hizo mbili, katika Wilaya za Kirehe na Kayonza, na pia kutembelea Hifadhi ya Akagera.

Bagabo John