Utawala wa Rais Donald Trump umekusudia kupunguza wafanyakazi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na kufikia 294
Utawala wa Rais Donald Trump umekusudia kupunguza wafanyakazi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) na kufikia 294 pekee kati ya jumla ya zaidi ya wafanyakazi 10,000 walioko duniani kote.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani bado haijatoa tamko kuhusu suala hilo.

Aliyewahi kuwa Mkuu wa USAID kwa zaidi ya miaka sita, J. Brian Atwood amesema uamuzi wa kuwafuta kazi wafanyakazi wengi, utaua shirika ambalo limeokoa mamilioni ya watu kote duniani.
