Katika hotuba yenye uzito mkubwa kwenye Kongamano la wanachama Cha Kisiasa Cha RPF-Inkotanyi, kilicho fanyika Tarehe 17 July 2026, Rais Paul Kagame alitoa msimamo mkali kuhusu kuongezeka kwa mvutano katika eneo la Maziwa Makuu pamoja na vikwazo vinavyoendelea kuwekwa na mataifa ya Magharibi., Akasisitiza kuwa Rwanda haitanyamaza.
Hotuba hiyo iligusia kwa uwazi hali halisi ya kisiasa na kiusalama inayolikabili Rwanda na eneo la Maziwa Makuu.
Kuhusu Amani ya Kanda:
Rais Kagame aliikosoa vikali uongozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), akidai unaendelea kuunga mkono kundi la waasi la FDLR badala ya kutafuta suluhisho la kweli la kuleta utulivu na amani.
Kuhusu Shinikizo la Kimataifa:
Alikataa kwa nguvu mkakati wa mataifa ya Magharibi wa kuanza kwa kuweka vikwazo ("sanctions-first approach"), akisema mataifa hayo hayapo tayari kusikiliza taarifa na tathmini za kiusalama zinazotolewa na Rwanda.
Kuhusu Viwango Viwili katika Haki za Binadamu:
Rais Kagame alieleza wasiwasi wake kuhusu kile alichokiita kupuuzwa kwa ukatili unaofanyiwa jamii za wachache mashariki mwa DRC, akisisitiza kuwa Rwanda haitanyamaza wakati watu wanalengwa kwa misingi ya utambulisho wao.
Bagabo John
