Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye pia ni mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesimamia mazoezi ya mwisho ya gwaride ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya sherehe ya kuapishwa kwa rais mteule wa nchi hiyo.
Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika Mei 12, 2026 katika viwanja vya Kololo mjini Kampala, ambapo Rais Yoweri Museveni ataapishwa rasmi kuendelea kuiongoza Uganda kwa muhula wake wa saba madarakani.
Mazoezi hayo yamehusisha vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na maandalizi ya mapokezi ya wageni wa kitaifa na kimataifa watakaohudhuria hafla hiyo muhimu ya kisiasa nchini Uganda.

Jenerali Muhoozi amesema maandalizi yanaendelea vizuri huku akisisitiza umuhimu wa nidhamu, umoja na usalama katika kuhakikisha shughuli hiyo inafanyika kwa mafanikio makubwa.
Kuapishwa kwa Museveni kunatajwa kuwa tukio muhimu katika historia ya kisiasa ya Uganda kutokana na muda mrefu aliokaa madarakani tangu mwaka 1986.
Bagabo John
