Rais Paul Kagame aliwakosoa viongozi wasiotimiza wajibu wao, akisema kuwa hali hiyo inasababishwa na tabia mbaya, hasa Majivuno na kujisifu bure hata wanapochukua hatua zisizo na msingi wowote.
Alirejelea hayo alipokuwa akifunga mkutano wa mashauriano wa viongozi wa taasisi za serikali na serikali za mitaa uliofanyika katika Chuo cha Kijeshi cha Gako, uliowahusisha viongozi wa wilaya, mawaziri mbalimbali na wengine.
Alisema, “Sababu kuu ni kuwa mna tabia mbaya, ikiwemo Majivuno na kujisifu bire, tabia hii mtaiharibu nchi yenu. Nyinyi ni wenye kiburi na mnajisifu bure. Mnajisifia nini? Ninyi viongozi mliopo hapa mnajisifia nini?”

Rais Kagame aliongeza kuwa ikiwa viongozi wamekubali kushika nafasi za uongozi, hawapaswi kukwepa wajibu wao; wanapaswa kuutekeleza au, ikiwa hawaoni thamani yake, waende wakafanye mengine wanayopenda.
Rais alisema kuwa huona mambo kwenye mitandao ya kijamii ambapo wananchi hulalamika; kisha huwatumia viongozi husika akiwauliza ni nini kinaendelea, lakini humjibu kuwa hawajui.

Akashangaa jinsi wasivyoweza kujua yanayotokea katika maeneo yao.
Bagabo John
