•     

Museveni amemteua tena Mkewe kuwa Wazili

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amemteua tena mkewe Janet Museveni kuwa Waziri wa Elimu katika Baraza jipya la Mawaziri lililotangazwa, huku sura nyingi mpya zikijumuishwa Serikalini.

Katika mabadiliko hayo, Makamu wa Rais Jessica Alupo pamoja na Waziri Mkuu Robinah Nabbanja wameendelea kubaki katika nafasi zao serikalini.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi waliodumu kwa muda mrefu wameondolewa kwenye Baraza hilo la Mawaziri. 

Miongoni mwao ni aliyekuwa Waziri wa Fedha Matia Kasaija pamoja na Naibu waziri mkuu Mkongwe Moses Ali.

Hatua hiyo inaonekana kama sehemu ya juhudi za Museveni kuhuisha serikali yake kwa kuingiza viongozi wapya huku akihifadhi baadhi ya watu wake wa karibu katika nafasi muhimu za uongozi.

Bagabo John