Mwamuzi Nsengiyumva Jean Paul baada ya kuonekana na tabia isiyofaa ya kumpiga teke mchezaji wa Mukura Victory Sports katika mechi iliyowakutanisha na Rutsiro FC., Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) limemfungia kipindi cha mwaka mmoja bila kuchezesha Mechi.
Ripoti ya Kamati ya Usimamizi wa Waamuzi imethibitisha kuwa mwamuzi Nsengiyumva Jean Paul alifanya makosa makubwa, yakiwemo mwenendo usioendana na majukumu yake (comportement incompatible avec sa fonction), baada ya kuonekana akimpiga teke beki wa Mukura Victory Sports, Mbonyamahoro Serieux, aliyekuwa akimfuata ili kuomba ufafanuzi kuhusu maamuzi yaliyotolewa.

Mchezaji wa timu ya Mukura Victory Sports, Mbonyamahoro Serieux, alie pigwa teke na Refa
Kutokana na tabia hiyo inayokiuka sheria na maadili ya soka, Nsengiyumva Jean Paul alipewa adhabu ya kusimamishwa kwa miezi 12 bila kuchezesha mechi, pamoja na kuongeza michezo mitano ya adhabu kutokana na makosa ya kiufundi aliyofanya katika mechi hiyo.
Adhabu hizi zinatarajiwa kuwa funzo kubwa kwa waamuzi wote, wakitakiwa kuzingatia weledi na kuepuka vitendo vinavyoweza kuharibu taswira ya mashindano ya Rwanda Premier League.

Refa Nsengiyumva Jean Paul Amesimamishwa Mwaka Mmoja bila Kuchezesha Mechi
Katika malalamiko yake, Mukura Victory Sports ilieleza kutoridhishwa na uamuzi wa mwamuzi, ikiwemo penalti mbili zilizotolewa kwa Rutsiro FC ambazo haikukubaliana nazo, pamoja na kuonyesha kuwa kulikuwa na unyanyasaji dhidi ya mchezaji wake—mambo ambayo baadaye yalithibitishwa na uchunguzi uliofanywa na FERWAFA.

Bagabo John
