•     

Tanzania: Raia washambulia askari wakihisi ni watekaji

Watu wawili, akiwemo askari polisi, wamejeruhiwa vibaya baada ya kushambuliwa na kundi la watu wakati polisi walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa aliyeingia nchini kinyume na sheria.

Raia washambulia askari wakihisi ni watekaji

Katika Kijiji cha Kirungu, Kata ya Janda mkoani Kigoma ,Polisi wameeleza kuwa tukio hilo lilitokea baada ya kumfanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Hata hivyo, mara baada ya kukamatwa, kundi la watu liliingia ghafla na kuzuia polisi kuondoka na mtuhumiwa huyo.
Kundi hilo liliwageukia askari na kuwashambulia kwa kutumia mawe pamoja na silaha za jadi wakihisi ni watekaji, na hivyo kusababisha majeraha kwa askari mmoja na mtu mwingine aliyekuwepo eneo hilo.

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limeeleza kuwa linachukua hatua za kuwafuatilia na kuwakamata wale waliotenda kitendo hicho cha kuwashambulia maafisa wa umma wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Bagabo John