Asasi za kiraia na taasisi za watetezi wa haki za binadamu 14 leo Aprili 27 zimekosoa ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Uvunjifu wa Amani wa Oktoba 29, 2025 wakitaka kuundwa kwa tume huru ya kimataifa na kuwalipa fidia waathirika wa vurugu hizo.
Asasi za kiraia na taasisi za watetezi wa haki za binadamu 14 leo Aprili 27 zimekosoa ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa Uvunjifu wa Amani wa Oktoba 29, 2025 wakitaka kuundwa kwa tume huru ya kimataifa na kuwalipa fidia waathirika wa vurugu hizo.
Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu, Mohamed Othman Chande ilikapbidhi ripoti hiyo Aprili 23 kwa Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu ya Dar es Salaam.
Taasisi hizo ni pamoja na Legal and Human Rights Centre (LHRC), Tanganyika Law Society (TLS), Centre for Strategic Litigation (CSL), Twaweza EA, Affirmative action on Gender Equality Network (AGEN)-Tanzania, Tanzania Human Rights Defenders Coalition (THRDC), Tanzania Transparency Forum (TRAFO), Taasisi Mwenyeji, Kiutawala, wa Tanzania Governance Multi-Stakeholders Group (TG-MSG)
Jukwaa la Katiba Tanzania na Concern for Development Initiatives in Africa (ForDIA), Taasisi Mwenyeji, Kiutawala, wa Vuguvugu la Raia ni Sisi Tanzania.

Nyingine ni National Consortium of Civic Education in Tanzania (NACOCET), Muungano wa Vyama Vya Wavuvi Tanzania (FUO), Pastoralists Indigenous Non-Governmental Organizations Forum (PINGOS Forum), Centre Against Gender Based Violence (CA-GBV) na Tanzania Child Welfare (TCW).
Akieleza kasoro zilizojitokeza wakati wa ukusanyaji wa taarifa wa tume hiyo.
Mwakilishi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Halima Sonda alisema Tume hiyo ilitumia vyanzo rasmi (Polisi, vituo vya afya) ambavyo wakati mwingine vinalalamikiwa kuwa wahusika wakuu wa ukiukaji wa haki.
Polisi wanatuhumiwa kuingilia utendaji wa mahospitali na vituo vya afya.
Alisema pia tume hiyo imeshindwa kubainisha viongozi walioshindwa kufanyia kazi maoni ya wadau yaliyotolewa tangu mapema kabla ya uchaguzi ili kuzuia machafuko, huku pia ikishindwa kuwataja kwa uwazi watu waliohusika na amri za utekaji, mauaji, na upotezaji wa watu takriban 700.
Kuhusu makambi na mafunzo kwa waandamanaji, Sonda alisema ingawa tume imetaja uwepo wa makambi ya mafunzo kwa wahusika wa ghasia, imeshindwa kubainisha mafunzo hayo yalitolewa na nani na katika maeneo gani mahususi.
Bagabo John
