Maafisa wakuu wa serikali wamepuuzilia mbali uvumi juu ya afya ya Rais Paul Kagame, wakithibitisha kuwa yuko katika hali nzuri na kuchukua mapumziko ya kibinafsi ya kawaida.
Majibu hayo yanakuja huku kukiwa na wimbi la madai yasiyo na msingi kwenye mitandao ya kijamii, yakichochewa zaidi na watu wenye chuki, wakosoaji na wapinzani wa kisiasa, wakidai kuwa Rais ni mgonjwa sana au amefariki dunia.
Msemaji wa serikali, Yolande Makolo amekiambia chombo chahabari hapa nchini kuwa uvumi huo hauna msingi wowote na akawataka wananchi kuwa watulivu.
"Tafadhali habari hizi ni za uwongo za chuki za mara kwa mara, msiwe na wasiwasi." alisema.

Msemaji wa serikali, Yolande Makolo
Ameendelea kusema kuwa Rais Kagame
yeye ni binadamu, na kama mtu mwingine yeyote, yeye huchukua muda kupumzika.
Leo hii Jeshi la Rwanda limekanusha taarifa iliyosambaa usiku wa manane kuhusu afya ya Rais Paul Kagame", ambapo jeshi la Rwanda lilisema ni Fake News.
Bagabo John
