Rais wa Jamhuri ya Rwanda na Amiri Jeshi Mkuu, Paul Kagame, amewatunuku cheo cha Assistant Inspector of Police (AIP) maafisa wadogo 436 waliohitimu mafunzo ya kujiunga na Polisi ya Rwanda, katika hafla iliyofanyika katika Chuo cha Polisi cha Gishari.
Maafisa hawa wapya wamejiunga na Polisi ya Rwanda baada ya kukamilisha mafunzo maalum yaliyowapa ujuzi wa kulinda usalama wa watu na mali zao.

Katika mafunzo hayo, walifundishwa matumizi ya teknolojia ya kisasa, mbinu za kupambana na uhalifu pamoja na usimamizi wa usalama kwa viwango vya kisasa.
Miongoni mwa waliohitimu mafunzo hayo, wanawake ni 109 huku wanaume wakiwa 327.
Pia kulikuwa na washiriki wa kigeni waliotoka nchini Seychelles.





Inatarajiwa kuwa maafisa hao watapangiwa kazi katika vitengo mbalimbali vya Polisi ya Rwanda, ikiwemo kitengo cha usalama barabarani, kitengo cha teknolojia, zimamoto pamoja na vitengo vingine vya usalama.
Bagabo John
