•     

Waandishi wa habari waliouawa wakati wa Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994 wamekumbukwa.

Waziri wa Umoja wa Kitaifa na Uraia, Dkt. Bizimana Jean Damascène, amesema kuwa vyombo vya habari vilichangia kwa kiasi kikubwa kuwahamasisha Wahutu kuwaua Watutsi na kueneza chuki iliyosababisha Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watutsi.

Alirejelea hayo jioni ya tarehe 10 Aprili 2026, wakati Waandishi wa habari na viongozi wa vyombo mbalimbali vya habari vinavyofanya kazi nchini Rwanda walipokuwa wakikumbuka kwa mara ya 32 Mauwaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka 1994

Waziri Dkt. Bizimana alieleza kuwa kulikuwa na makundi tofauti ya vyombo vya habari, yakiwemo vya Serikali, vile vilivyojiita huru lakini vikashirikiana na Serikali, na vile huru vilivyotumika kueneza chuki.

Waziri wa Umoja wa Kitaifa na Uraia, Dkt. Bizimana Jean Damascène.

Aliongeza kuwa Radio Télévision Libre des Mille Collines iliajiri wanahabari wenye ujuzi pamoja na baadhi ya waliokuwa viongozi, ili kuijengea uwezo wa kufanikisha ajenda mbaya ya kisiasa ya chuki miongoni mwa Wanyarwanda.

Alibainisha pia kuwa wanahabari mbalimbali waliokuwa wafanyakazi wa ORINFOR, Imvaho, Kangura, Kinyamateka na vyombo vingine vya habari walihusika katika kueneza chuki.

Alieleza kuwa ili kuhakikisha Radio Télévision Libre des Mille Collines zisipoteze  mwelekeo wake, mtandao wake wa matangazo uliunganishwa na ule wa Ikulu ya Rais wa Jamhuri kutokana na umuhimu uliokuwa ukipewa.

Aidha, alionyesha kuwa baadhi ya viongozi wa Serikali waliwekwa katika bodi za uongozi za RTLM, huku wakiendelea pia kushikilia nyadhifa zao serikalini.

Bagabo John 