•     

Ruto ampongeza Samia kwa kuunda Tume ya Chande

Rais wa Kenya, William Ruto, amemmiminia sifa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kuunda Tume ya Jaji Othman Chande, akitaja hatua hiyo kama kielelezo cha juu cha ukomavu wa kisiasa. Ruto amesema kuwa hatua ya kuchunguza uvunjifu wa amani wa kipindi cha Uchaguzi Mkuu 2025 ni darasa tosha kwa viongozi wa ukanda wa Afrika Mashariki.

​Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mei 4, 2026, Rais Ruto amebainisha kuwa ujasiri wa kutafuta ukweli kupitia tume huru ndiyo njia pekee ya kuimarisha misingi ya haki na utawala bora kwa mataifa yanayochipukia kidemokrasia.

​“Kuundwa kwa tume hii kunaonesha dhamira ya dhati ya Rais Samia katika kutafuta ukweli wa kilichotokea na kuhakikisha masuala yote yanayohusu amani na utulivu yanapatiwa ufumbuzi wa kudumu ndani ya mipaka ya nchi,” amesema Rais Ruto.

​Aidha, kiongozi huyo wa Kenya amesisitiza kuwa Kenya na nchi nyingine za Afrika Mashariki zinaunga mkono mchakato huo, kwani amani ya Tanzania ndiyo uti wa mgongo wa utulivu wa kikanda. Amesema kuwa uzoefu wa Kenya unaonyesha kuwa hatua kama hizo husaidia mataifa kuibuka yakiwa imara zaidi na yenye mshikamano wa kitaifa.

Tume hiyo ya Jaji Othman Chande inatarajiwa kufanya tathmini ya kina juu ya matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Rais Samia ya kuhakikisha maridhiano na haki vinatawala katika uongozi wake.

Bagabo John 