•     

Ushirikiano wa Wananchi wajenga Rwanda Imara na yenye Umoja

Kamishna Mkuu wa FPR Inkotanyi, Balozi Christophe Bazivamo, katika Kongamano la wanachama Cha RPF Inkotanyi Tarehe 17 July 2026 alitoa hotuba akisisitiza kuwa kila mwanachama wa FPR Inkotanyi ana jukumu muhimu katika ujenzi na maendeleo ya Rwanda.

Alieleza kuwa mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 32 tangu ukombozi wa nchi hayakutokana na juhudi za viongozi pekee, bali yalitokana na mchango wa kila mwanachama na kila raia aliyeshiriki kwa dhati katika kujenga taifa lenye umoja, amani na maendeleo.

Bazivamo alisema kuwa katika kipindi chote hicho cha miaka 32, Rwanda imepiga hatua kubwa kutokana na misingi imara iliyowekwa na uongozi pamoja na wananchi. 

Alifafanua kuwa safari ya ujenzi wa taifa imejengwa juu ya kuimarisha umoja wa Wanyarwanda, kuhimiza utamaduni wa mazungumzo na majadiliano katika kutafuta suluhisho la changamoto mbalimbali, pamoja na kujenga mazingira ya usalama na utulivu yanayowezesha maendeleo endelevu.

Aidha, alisisitiza kuwa maendeleo ya Rwanda yameongozwa na dhana ya umiliki wa kitaifa (national ownership), ambapo wananchi wenyewe wanashiriki kikamilifu katika kupanga, kutekeleza na kulinda mipango ya maendeleo ya nchi yao bila kutegemea wengine. Kwa mujibu wake, mtazamo huo umeifanya Rwanda kujitegemea zaidi na kuhakikisha mafanikio yaliyopatikana yanadumu na kuendelea kuwanufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.

Katika hotuba yake, Balozi Bazivamo pia alieleza kuwa ari ya kujitolea na kujituma kwa wanachama wa FPR Inkotanyi inaendelea kuwa nguzo muhimu katika kuharakisha maendeleo ya taifa. 

Alisema kujitolea huko kumechangia kuimarisha utawala bora, huduma kwa wananchi, mshikamano wa kitaifa na utekelezaji wa sera mbalimbali za maendeleo.

Akihitimisha, alionesha kuridhishwa na fursa ambazo wanachama na wananchi wamepewa kushiriki katika maendeleo ya nchi. 

Aliwahimiza kuendelea kulinda umoja, amani, usalama na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 32 iliyopita, ili Rwanda iendelee kuwa taifa lenye maendeleo, uthabiti na ustawi kwa vizazi vijavyo.

Bagabo John