•     

Dkt. Frank Habineza amesema Upinzani nchini Rwanda si vita wala kuharibu mafanikio ya wananchi

Seneta Dkt. Frank Habineza, ambaye pia ni Msemaji wa Jukwaa la Vyama vya Siasa vinavyotambuliwa nchini Rwanda, amesema kuwa kuna vyama mbalimbali vyenye misimamo huru, na kwamba tofauti zao za maoni si mapambano wala kuharibu mafanikio yaliyopatikana katika miaka 32 iliyopita.

Amesema hayo hii leo  tarehe 13 Aprili 2026, wakati wa hafla ya kuwakumbuka kwa mara ya 32 wanasiasa waliouawa katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi.

Hafla hiyo iliendana na hitimisho la wiki ya maombolezo, iliyofanyika Rebero, mjini Kigali, katika kumbukumbu inayohifadhi miili ya wanasiasa 21 waliouawa kwa kupinga ubaguzi uliopelekea mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994

Seneta Dkt. Habineza amesisitiza kuwa vyama 11 vya siasa nchini Rwanda vina mitazamo tofauti na vinafanya kazi kwa amani ndani ya taasisi za uongozi wa nchi, huku kila chama kikiendelea kushikilia msimamo wake wa kisiasa.
Alisema, “Vyama vyote 11 vya siasa vinawakilishwa katika Bunge na katika taasisi nyingine za uongozi wa nchi. Ieleweke wazi kuwa kukutana na kujadiliana kuhusu masuala ya kitaifa hakuondoi uhuru wa kila chama cha siasa.”

Alisema, “Hali hii haizuii kila chama cha siasa kuwa na mtazamo wake tofauti na kingine, jambo ambalo wengine huliita ‘upinzani’. Kutokubaliana na serikali nchini Rwanda si vita wala kuharibu mafanikio yaliyopatikana baada ya miaka 32 tangu mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka 1994.

Upinzani wetu ni kutoa mawazo na kutafuta suluhisho kwa changamoto zilizopo, huku tukizingatia historia mbaya ambayo Rwanda imepitia.”

Akizungumzia kipindi cha maombolezo ambacho nchi inapitia, Dkt. Habineza alisema kuwa bado kuna Wanyarwanda walioko uhamishoni, wakiwemo waliokwenda kama wakimbizi na wengine waliohusika katika Mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka  1994,  wakiwemo baadhi ya waliokuwa wapiganaji wa FDLR.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa sera ya Rwanda ni kwamba hakuna raia anayepaswa kubaki uhamishoni.

Bagabo John