•     

Mh. John Wegese Heche, amezuiliwa na maafisa wa uhamiaji

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. John Wegese Heche, amezuiliwa na maafisa wa uhamiaji katika mpaka wa Tanzania–Kenya, eneo la Sirari, Wilaya ya Tarime, wakati akielekea nchini Kenya kuhudhuria mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Hayati Raila Amolo Odinga.

Mh. John Wegese Heche, amezuiliwa na maafisa wa uhamiaji katika mpaka wa Tanzania–Kenya

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Katibu wa Kanda ya Serengeti, J. Mnyawami, maafisa wa uhamiaji walichukua hati ya kusafiria ya Mh. Heche na hawajatoa maelezo yoyote kuhusu sababu za kumzuia kuvuka mpaka.

Tukio hili limeibua maswali miongoni mwa wananchi na wafuasi wa chama hicho, hasa ikizingatiwa kuwa jana serikali ya Tanzania iliwakilishwa rasmi katika ibada ya kitaifa ya kuuaga mwili wa Odinga iliyoandaliwa Uwanja wa Nyayo, Nairobi.

Wawakilishi wa Tanzania katika ibada hiyo waliongozwa na Makamu wa Rais, Mh. Dkt. Philip Mpango, wakishirikiana na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine waandamizi wa serikali.

Kwa sasa, chama kimesema kinaendelea kufuatilia kwa karibu hali hiyo, na taarifa rasmi kutoka Makao Makuu ya CHADEMA zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni.

  Bagabo John 